Thursday, 23 May 2013

KWA TAARIFA YAKO : ASKOFU GWAJIMA ALIPOOZA KWA MIAKA 6 KITANDANI KABLA YA KUWA MCHUNGAJI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.



KWA TAARIFA YAKO wiki hii mdau wetu ni kwamba yawezekana umekuwa ukisikia mambo mengi yanayotendeka katika kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na askofu Josephat Gwajima makao makuu yake yakiwa Kawe Tanganyika Packers jijini Dar es salaam, kanisa hili limekuwa maarufu sana kwa jinsi Mungu ambavyo amekuwa akimtumia mchungaji kiongozi na mwanzilishi wa huduma hiyo Josephat Gwajima  kuombea na kuwarudisha kwa jina la Yesu watu waliokufa katika mazingira ya kutatanisha au kimazingara ambao kwa ushuhuda wengi wao kwasasa wamekuwa waumini wa kanisa hilo.

Kama hujui kuhusu mchungaji Gwajima ni kwamba akiwa na umri wa miaka 10 alipata ajali iliyompelekea kupooza kwa miaka sita na madaktari wakithibitisha kwamba kwa hali haliyokuwa nayo asingeweza kurudia katika hali yake ya kawaida tena, kwahiyo akawa kitandani aliyesubiri kuletewa huduma zote, baada ya miaka sita kitandani usiku mmoja Yesu Kristo alimtokea mchungaji Gwajima ndotoni na kumwita kwa jina lake na kumsimamisha kutoka kitandani, ambapo alipozinduka katika ndoto hiyo usiku huohuo alijaribu kusimama kutoka kitandani akaona ameweza akajaribu kupiga hatua akaona zinapigika akatoka nje na kuanza kumwita baba yake mzazi na ndugu zake ambao hawakuamini kumuona akitembea, usiku huo alimpa Yesu Kristo maisha yake na kuitiwa utumishi shambani mwa Bwana.
Askofu Gwajima na mkewe pastor Grace Gwajima.
KWA TAARIFA YAKO kanisa hili pia limekuwa maarufu sana kutokana na kifo cha aliyekuwa mtabiri maarufu wa nyota Afrika mashariki na kati marehemu sheikh Yahya Hussein ambaye kifo chake cha wezekana kisingetokea kwa wakati ule kama angelisikia na kufuata lile aliloambiwa na mchungaji Gwajima aliyemtaka shehe huyo kujisalimisha kanisani kwake na kueleza bayana anayoyafanya ndio itakuwa salama yake la! ndani ya miezi mitatu asipofanya hivyo atakufa na ndivyo ilivyotokea ( ushuhuda huu tutakuja kuuandika kwa kina siku za mbeleni).

Baadhi ya waumini katika kanisa hilo.

Lakini kama haitoshi KWA TAARIFA YAKO kanisa hili lililochini ya mchungaji Gwajima ndilo linaloongoza Afrika mashariki na kati kwakuwa na waumini wengi wanaohudhuria ibada kwa siku za jumapili lakini pia yawezekana bado linashika nafasi hiyo kwa ibada za katikati ya wiki. Lakini pia kanisa hili kwasasa linaongoza kwakuwa na waimbaji wengi binafsi ambao wamevumbuliwa na mpango kabambe uliowekwa na mchungaji Gwajima uliopewa jina la Viliba. KWA TAARIFA YAKO kama hujui Martha Mwaipaja ametokea katika kanisa hili na alikuwa akisapotiwa na mchungaji Gwajima kama anavyofanya kwa waimbaji wengine wa kanisa hilo, ingawa kwasasa Martha ashiriki tena kanisani hapo baada ya kuolewa na mchungaji John Said kwasasa nayeye ni mama mchungaji.

WANAUME JELA MIAKA 6 NA VIBOKO 300 KWAKUMBADILISHA DINI MWANAMKE

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia.
Mahakama moja huko Riyadh nchini Saudi Arabia imewahukumu wanaume wawili kwenda jela kwakosa la kumbadilisha dini mwanamke wa kiisalmu kuwa Mkristo pamoja na kumsaidia mwanamke huyo kuondoka nchini humo jambao ambalo ni kinyume na sheria za nchi hiyo inayoongozwa kwa misingi ya dini ya kiislamu.

Wanaume hao mmoja ambaye ni Mlebanon amehukumiwa miaka sita jela pamoja na viboko 300 kwakosa la kumbadilisha dini mwanamke huyo huku mwanaume mwingine ambaye ni raia wa nchini hiyo amehukumiwa miaka miwili jela pamoja na viboko 200 kwakosa la kumsaidia mwanamke huyo kutoroka nchini humo ingawa inadaiwa watuhumiwa hao wanampango wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo

Nchini Saudi Arabia ambako ndiko kuna aminika dini ya kiisalmu kuwa chimbuko lake ni kosa la jinai kuikana dini hiyo na kujiunga na dini nyingine ikiwa pamoja na kutangaza dini hizo hadharani pia ni kosa la jinai. Kwa mujibu wa familia ya mwanamke aliyebadilishwa dini, wamelalamika kuwa mwanamke huyo ametekwa mawazo na wafanyakazi wenzake katika kampuni ya bima alikokuwa akifanya kazi na hatimaye kufanikiwa kutoroka kwa nyaraka bandia kupitia Bahrain na hatimaye kupata makazi ya ukimbizi nchini Sweden.

CHANZO BONYEZA HAPA

VIZUIZI VYA KUSHINDWA KUFANYA HUDUMA YA MUNGU IPASAVYO.* sehemu ya tatu*

Mtumishi Gaper Madumla.
Kumbuka kwamba tunachoangalia katika fundisho hili ni sababu za msingi zinazowafanya watumishi au mkristo yeyote Yule kushindwa kufanya kazi ya Mungu ipasavyo.

Sababu hizo zinazomzuia au kumfanya mtu aliyeyebeba huduma ya Mungu isiweze kuifanya katika viwango vya juu.
Sababu hizi hujulikana kama VIZUIZI au VIKWAZO.
Basi sasa nianze kwa kukusalimu wewe mpendwa,nikikuambia,

Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya…

Karibu sasa tuendelee na fundisho letu.
Kumbuka tulikoishia katika sehemu ya pili.
Kupitia kitabu cha Mathayo 17 :14-21
Tulifanikiwa kubainisha sababu/Vikwazo viwili vinavyotupelekea kushindwa kuhudumu vizuri kwa habari ya kazi ya Bwana katika shamba lake.

Sababu hizo ni :
01. Upungufu wa imani.
02. Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba.

Tulijifunza kiundani moja wapo ya sababu /Kizuizi kinachomfanya mtu wa Mungu kushindwa kutekeleza huduma ya Mungu iliyomo ndani yake.
leo tunaendelea kuchambua sababu hiyo ambayo ni :

01.UPUNGUFU WA IMANI.

( Kwa maelezo ya awali ,tafadhali tafuta sehemu zilizopita )
“ Yesu akawaambia, Kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI yenu.
Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” Mathayo 17 :20

• IMANI inapokuwa ni pungufu kwa mkristo anayefanya huduma,Basi ujue hawezi kupata mpenyo.
Mfano kama mtu huyo mwenye imani pungufu akiwa ni muombaji,Basi ujue hakuna uponyaji utakaotokea baada ya maombi yake.

Tuendelee kutazama habari hiyo ya wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kufanya huduma kwa sababu ya kuwa na upungufu wa IMANI.
Tunaona Yesu akajibu, akasema, :

“ Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. ” Mathayo 17 :17-18

Mgonjwa yule alipoletwa kwa Yesu ,
Yeye Bwana Yesu hakutumia nguvu ya kumkemea kama walivyofanya wale wanafunzi wake,
Bali alimuamuru pepo mchafu amtoke Yule kijana, naye huyo pepo akamtoka saa ile ile.

Nalipenda andiko hilo katika Biblia ya Bible in Basic English (BBE) Andiko hilo linasema hivi : “And Jesus GAVE ORDERS to the unclean spirit, and it went out of him: and the boy was made well from that hour.” Matthew 17 :18

Alichokifanya Bwana Yesu ni kutoa TAMKO/AGIZO juu ya Yule pepo.
Bwana Yesu alikuwa haitaji kutumia nguvu zake kwa kijipepo hicho.
Ilikuwa ni rahisi sana kwa Bwana Yesu kutoa pepo,na wala si tu kwa sababu Yeye ni mfano wa Mungu Baba la hasha!

Bali pia Yeye alijaa IMANI KAMILI na hii ndio sababu ya msingi,maana wanafunzi waliposhindwa kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI Yeye Bwana Yesu akaweza kwa sababu ya kuwa na IMANI ILIYOKAMILI.
Hapo tunajifunza kuwa,haitajiki kumkemea pepo muda mlefu pasipo majibu,Bali tunahitajika kutoa AGIZO lenye utiisho ndani yake juu ya kila aina ya mapepo na ufalme wao wa giza.

Wednesday, 22 May 2013

PCT WATOA TAMKO KUPINGA UPOTOSHAJI, KUHUSU MIKUTANO YA INJILI

Lifuatalo ni tamko la Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste ambalo limetolewa tarehe Jumatano 22 Mei 2013, kupinga upotoshaji unaoenezwa kuhusu maazimio ya kikao cha majadiliano ya viongozi wa dini na serikali Dar es Salaam tarehe 7-8 Mei 2013.



MAKALA : IJUE HISTORIA YA ASKOFU MOSES KULOLA AMBAYE ANAONGOZA MAKANISA 4000


Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.


Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.


Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.

Askofu Kulola aliyeketi akiwa na waimbaji wa injili nchini Mwinjilisti Faustin Munishi mkono wa kushoto pamoja na Emmanuel Mwasota. mwanzoni mwa mwaka 1970
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

Tuesday, 21 May 2013

MAMBO HAYAJILETI YENYEWE - MAMBO YANASABABISHWA KUTOKEA.


Na Mwalimu Alfred Katuma.

5 Naam ,na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu,
Katika imani yenu tieni na wema na katia wema wenu maarifa……….”.
(1pet.1:5)
Bwana akufunulie akili zako ili uelewe hiki tunachojifunza lakini pia akusaidie kuyaweka kwenye matendo haya unayojifunza. Sasa hivi tunaishi kwenye nyakati ambazo kumezuka mafundisho yenye msisitizo mkubwa sana kwenye upande mmoja wa miujiza kiasi kwamba watu wengi sana wamejikuta wanaishi maisha ya kimiujiza miujiza,naamanisha watu wamekuwa wanaishi wakitegemea kufanikiwa katika maisha kwa miujiza tu unakuta mtu hataki kufanya kazi anategemea akienda kuwekewa mikono na watumishi basi mambo yatajileta yenyewe tu! Kwa sababu ya watu wengi kutaka kuishi kimiujiza wamejikuta kila kitu wanaita muujiza, unakuta mtu kafanikiwa kununua gari eti anaita muujiza au mtu kwenda ulaya anaita muujiza, mama kanunuliwa kanga na mumewe anaita muujiza. 

Sijui kwa nini nimeanza kwa style hii lakini ninamini kuna kitu Mungu anataka tujifunze hapa na nianze kuelezea  kuhusu muujiza. Ukisoma katika kamusi ya Kiswahili sanifu inafafanua neno muujiza kama jambo lisilokuwa la kawaida. Kwa maana  nyingine muujiza ni matendo yanayofanyika kinyume na maumbile ya asili ni mambo ambayo hata ukimwambia mwanasayansi afafanue hawezi kuyafafanua yametokeaje, lakini utakuta mtumishi wa  Mungu anamuombea mtu anasema ,”pokea muujiza wa kwenda ulaya! Pokea muujiza wa gari pokea muujiza wa nyumba! Na maombi mengine mengi ambayo ninaamini msomaji unayafahamu au umeshawahi kuombewa. Nisikilize nikwambie kama hayo maombi unayoombewa yangekuwa yanatokea, mfano unaambiwa pokea muujiza wa gari halafu gari inatokea from no where au ukienda nyumbani unaikuta gari imepark hujui ilikotoka haina mwenyewe basi huo ndo muujiza lakini ukichukua hela ukaenda mwenyewe kununua gari hapo kuna muujiza gani ndugu? Au unaombewa pokea muujiza wa kwenda ulaya halafu ghafla unajikuta uko ulaya hujui umefikaje huo nao ni muujiza. 

Kitu gani nataka ujifunze hapa? Uache kuishi maisha ya kimiujiza kwa sababu mambo hayajileti yenyewe yanasababishwa kutokea,utanielewa tu huko mbele! Angalia Biblia yako nikuonyeshe mifano michache kuhusu miujiza halafu tuendelee, kutoka  7:10-12 inasema,

10………Haruni akabwaga fimbo yake chini mbele ya farao,mbele ya watumishi wake,ikawa nyoka.
11Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi;na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo 
Kwa uganga wao. 12Wakabwaga kila mtu fimbo yake,nazo zikawa nyoka;lakini fimbo ya Haruni
Ikazimeza fimbo zao”.

Sikia! hata ungewaita wanasayansi hapo hakuna ambaye angekueleza ile fimbo ya musa na za wachawi ziligeuka vipi zikawa nyoka! Huo ulikuwa muujiza lakini nataka ujifunze mambo machache hapa, kwanza fahamu Mungu anatenda miujiza lakini pia kama hufahamu shetani naye anatenda miujiza! Umeona hapo fimbo ya Musa ilipotupwa chini iligeuka nyoka na wachawi wa farao wakatupa zao nazo zikawa nyoka lakini (naupenda sana huu mstari) fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zile za wachawi! Unajua maana yake? Ni hivi, kile kitendo cha fimbo ya Haruni kumeza fimbo za wachawi Mungu alikuwa anamaanisha kwamba yeye ni mkubwa kuliko shetani,alikuwa anamaanisha muujiza wake ni mkubwa na unadumu kuliko wa shetani! 

Ngoja niishie hapo Mungu akitoa nafasi nitakuja na somo linalohusiana na miujiza na Baraka maana hivi ni vitu vinavyowasumbua sana watu kiasi cha kuwafanya waishi maisha ya kutanga tanga kwa kuhama kanisa hili kwenda kanisa jingine. Sasa angalia maneno anayosema Mtume Petro wakati analiandikia kanisa waraka wake wa kwanza na ninachotaka uone hapo ni yale maneno anayosema “mkijitahidi kwa UPANDE WENU”!  Sijui kama umeshawahi kutafakari mstari huu kwa makini na ukangundua yaliyojificha hapo; Petro anaposema kwa upande wenu ina maanisha kuna sehemu yako wewe kufanya kwa upande wako na kama kuna upande wako kufanya kitu basi  pia kuna sehemu ya Mungu kufanya kwa upande wake na  ndio maana kichwa cha somo kinasema mambo hayajileti  yenyewe kwa sababu kuna kitu unatakiwa kufanya kwa upande wako ambapo ukikiunganisha na upande anaofanya Mungu unapata jibu lako! Ngoja twende na mifano, angalia yeremia  29:12 – 14 inasema hivi:-
12 Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza.13 Nanyi mtanitafuta,na kuniona,mtakaponitafuta
Kwa moyo wenu wote.14 Nami nitaonekana,asema BWANA,nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa……………….”.

Kwa tafsiri rahisi ni kama Mungu anasema,kwa upande wenu mnachotakiwa kufanya ni kuniita,mnachotakiwa kufanya ni kuniomba na kwa upande wangu ninachotakiwa ni kuwasikiliza,na kujionyesha kwenu! Maana yake ni nini? Kama huiti Mungu hawezi kuitika! Ndiyo! Ataitikaje wakati hajaitwa? Mpendwa unakumbuka ule mstari ambao hata ukimuuliza mtu asiye na tabia ya kusoma biblia atakutajia mstari huo? Ni ule wa mathayo 7:7, hebu uangalie kwa namna hii nilivyofanya ili kukurahisishia kuelewa!
Upande wako kufanya kitu                                                  upande wa Mungu kufanya kitu
Ombeni nanyi (kuomba)                                                       mtapewa  (kukupa unachoomba)
Tafuteni nanyi (kutafuta)                                                      mtaona (kukuonyesha unachotafuta)
Bisheni nanyi   (kubisha/kupiga hodi)                                 mtafunguliwa (kukufungulia malango)

Kumbuka mambo hayajileti yenyewe bali yanasababishwa kutokea na kwasababu hiyo hauwezi kufanikiwa katika jambo lolote kama utakuwa ni mtu wa kukaa na kusubiri Mungu afanye kitu na hata kama Mungu akifanya kitu amefanya kwa upande wake kama wewe hujafanya  kwa upande wako hauwezi kupata matokeo! Angalia mfano huu nikuonyeshe kitu, fungua Yohana 9:6-7 inasema hivi,
6 Alipokwisha kusema hayo,alitema mate chini,akafanya tope kwa yale mate.
Akampaka kipofu tope za macho,7 akamwambia,nenda kanawe katika birika ya Siloamu,
(maana yake aliyetumwa).Basi akaenda na kunawa;akarudi anaona”.

Hii ni habari ya mtu mmoja aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa  na kwa bahati akakutana na Yesu lakini katika kuponywa kwake kuna kitu alitakiwa afanye kwa upande wake ili kukamilisha uponyaji wake na kilikuwa ni kwenda kunawa kwenye birika ya siloamu na biblia inasema akaenda na kunawa akarudi anaona! Kama yule kipofu angeamua kudharau akapitiliza na kuendelea na mambo yake mengine asiende kunawa ninakwambia angebaki kipofu hivyo hivyo lakini si kwa sababu Mungu hakufanya kitu,hapana, Mungu alishafanya kwa upande wake na ilibaki sehemu yake yule kipofu kufanaya ili kukamilisha uponyaji wake!
Okey! Angalia mfano wa mtu mmoja aliyekuwa na ukoma jina lake Naamani, huyu alimwendea mtumishi wa Mungu Elisha baada ya kusikia kuwa anaweza kumponya. Alipofika kwa Elisha,alitumiwa ujumbe wa mtu kumwambia kuwa aende katika mto Yordani akajichovye mara saba na ngozi ya mwili wake itarudi kuwa kawaida kabisa. 

Naamani aliposikia hivyo alikasirika na kusema,”Tazama,nilidhania,bila shaka atatoka kwangu, na kusimama na kuomba kwa jina la BWANA,Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa na kuniponya mimi mwenye ukoma. Je abana na farpari,mito ya Dameski si bora kuliko mito yote ya Israel? Siwezi kujiosha ndani yake na kuwa safi? Akageuka akaondoka kwa hasira”.
(soma habari hii katika kitabu cha 2wafalme 5:9-14) Haya ndiyo mwazo waliyonayo watu wengi sana wanapokwenda kanisani au kwenye semina na mikutano ya neno la Mungu au wanapofanyiwa maombezi. Unakuta mtu haamini mpaka awekewe mikono na mtumishi, lakini nataka nikwambie kitu kimoja ambacho watu wengi wamekuwa wanakosea ambacho ni kutokuafuata maagizo wanayopewa na watumishi au kutofuata vile neno linavyosema. Sikia! Kama umeambiwa kanawe katika birika ya siloamu nenda kanawe! Kama umeambiwa kajioshe kwenye mto yordani, nenda kajioshe! Kama umeambiwa endelea mbele hata kama mbele yako kuna bahari, wewe endelea mbele!!! JUST DO IT! Upande wa Naamani ulikuwa ni kujiosha kwenye mto Yordani tu na hakuna kingine na ndio maana wale watumishi walimwambia maneno haya,”Baba yangu kama yule nabii angelikuambia kutenda jambo kubwa,usingalilitenda? Je si zaidi basi akikuambia,Jioshe uwe safi?” nachotaka kukuambia hapa ni wewe kufuata maagizo ya neno la Mungu linavyosema. Kwa hiyo nabii Elisha alifanya kwa upande wake na ulibakia upande wa muhitaji ambaye ni naamani, na lipokubalikufuata maagizo alipona kabisa!(haleluya!) Petro anasema mkijitahidi kwa upande wenu, (kumbuka hilo). 

SHANGILIENI WAFANYA HUDUMA KUBWA HOSPITALI YA KCMC MOSHI

Kwaya kongwe nchini ya Tumaini Shangilieni kutoka kanisa la Mtakatifu James jijini Arusha, imefanya uinjilisti mkubwa usiku wa kuamkia jumamosi iliyopita katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro, waimbaji hao walitoa huduma kwa kugawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na kuwafariji na kuwaombea kwamba Mungu awaponye katika magumu wanayopitia.

Kati ya matukio ambayo yaliwasisimua waimbaji hao ni kumuona kijana mdogo ambaye amelazwa hospitalini hapo kwa takribani mwaka mzima baada ya kuungua vibaya kwa moto. Baada ya huduma hiyo hospitalini waimbaji hao waliungana na waimbaji wengine walioalikwa kwa tukio la mkesha wa uimbaji ulioenda sambamba na mdahalo kuhusu tasnia ya uimbaji uliofanyika katika kanisa la chuo, ambapo waimbaji waalikwa kama Abednego Hango wa New life band, Jackson Benty, mchungaji Mgondo wa Zion temple wote wa Arusha walihudhuria pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.

Baadhi ya waimbaji wa Tumaini wakiwa wamewasili hospitalini hapo tayari kwa huduma.






Walihitimisha kwa maombi mazito.
Kati ya majembe ya Tumaini choir, Wilson na uncle wake Emmanuel Mtangoo ambaye ni mwenyekiti wa kwaya wakikung'uta magitaa.
Tumaini wakimsifu Mungu. 

Emanuel Mtangoo mwenyekiti wa kwaya akionyesha mfano wa kucheza kwa Mungu wake.
Pastor Mngodo wa Zion Temple akizungumza jambo.

Abednego Hango wa Newlife Band akitoa mada kwenye mkesha huo.